Ezra 7:6-7

6 aHuyu Ezra alipanda kutoka Babeli. Alikuwa mwalimu mwenye ujuzi mzuri katika sheria ya Musa, ambayo Bwana, Mungu wa Israeli, alikuwa ametoa. Mfalme alikuwa amempa Ezra kila kitu alichoomba, kwa maana Bwana Mwenyezi Mungu wake alikuwa pamoja naye. 7 bPia baadhi ya Waisraeli, wakiwemo makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu na watumishi wa Hekalu,
Yaani Wanethini (pia 7:24).
nao walikuja Yerusalemu mwaka wa saba wa utawala wa Mfalme Artashasta.

Copyright information for SwhKC